Wanafunzi hao kutoka katika Klabu ya Wanafunzi ya Kutetea Haki za Binadamu walifika katika ofisi za TAMWA ili kuwasilisha pongeza zao hizo na kumtaka aendelee na juhudi zake za kuhamasisha umma dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TAMWA aliwashukuru wanafunzi hao kwa kutambua mchango wake na kwamba hatua hiyo inampa nguvu zaidi katika kupambana na changamoto wanazokutana nazo watoto na wanawake ikiwemo ndoa za utotoni, ubakaji na pia ukeketaji.
Aliongeza kuwa pamoja na changamoto za kijamii, mila na desturi, hakuna sababu ya mtoto wa kike kuolewe akiwa na umri mdogo kwa sababu ni kinyume cha haki za binadamu, zinamuondelea nafasi ya elimu na kujiendeleza kimaisha na kubwa zaidi ndoa hizo zinahatarisha maisha ya mtoto huyo ambaye mwili wake bado haujakomaa kuweza kujifungua.
Msoka alisema kwa nguvu za pamoja na ushirikiano wa kila mtu katika nafasi yake na vyombo vya habari kuendelea kuhabarisha na kuelimisha watanzania kuhusu athari za ndoa za utotoni hatimaye suala hilo litatokomezwa.
No comments:
Post a Comment