Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) leo kimezindua mradi mpya unaofadhiliwa na Sourthen African
AIDS Trust (SAT) unaolenga kukomesha
ongezeko la vitendo vya ubakaji na ulawiti katika wilaya ya Kinondoni na Temeke
mkoani Dar es salaam.
Mradi huo umezinduliwa na Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA Bi Edda Sanga katika Hoteli ya Elegancy iliyopo Sinza Mori Dar es
salaam.
Mwezeshaji katika uzinduzi wa mradi huo ni Bi Valerie Msoka ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Mtandao wa mashirika yanayopinga ndoa za utotoni(TECMN).
Uzinduzi huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo
waalimu, wanafunzi, madakatari, mahakimu, pamoja na viongozi wa Serikali za Mitaa kutoka wilaya
za Kinondoni na Temeke.
Aidha kupitia mradi huo, TAMWA itatumia vyombo vya
habari katika kutoa elimu ya masuala ya ubakaji na ulawiti kwa watoto ndani
ya jamii kwa kushirikiana na kitengo
chake cha usuluhishi cha TAMWA (CRC),
kinachotoa ushauri nasihi na msaada wa
kisheria.
No comments:
Post a Comment