Mtandao wa kutokomeza ndoa za utotoni Tanzania ‘TECMN’
umesikitishwa na kitendo cha baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kuunga mkono hoja ya kutowapa nafasi ya kuendelea na masomo
wanafunzi wa kike waliopata ujauzito wakiwa shuleni baada ya kujifungua.
Mwenyekiti wa TECMN, Valerie Msoka amesema kitendo
kilichofanywa na Wabunge kinarudisha nyuma jitihada mbalimbali zinazofanywa
katika kuleta usawa wa kijinsia na kumuinua mwanamke kijamii, kisiasa na
kiuchumi.
Aidha, ameongeza kuwa sababu mbalimbali zilizotolewa na
Wabunge ni za kisiasa zaidi kwa kuwa hazizingatii ustawi wa mtoto wa kike na
mustakabali wa maisha yake akisema Wabunge walioshabikia hoja hiyo
wamedhihirisha kutotambua viini vya matatizo yaliyomokatika jamii.
Mwenyekiti wa mtandao wa kutokomeza ndoa za
utotoni Tanzania(TECMN) Valerie N. Msoka akiongea na waandishi wa habari leo
mapema jijini dar es salaam kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa TAMWA Bi. Edda
Sanga.